
PUNGUZA MBWEMBWE LIMBUKENI WE! Muungwana hajitambulishi hivyo. Inatosha kabisa kusema: Mimi ni Makubi Masalakulanga, bila kusema "Mimi Bwana..." Anayekusikiliza atajua tu kwamba wewe ni bwana na wala si bibi. Iwapo ni muhimu kwa huyo unayezungumza naye kujua kwamba wewe ni waziri wa kitu fulani, hilo ni halali kutaja, lakini mbwembwe nyingine ni ulimbukeni mtupu. Pia ondoa hiyo 'lebo' kwenye mkono wa hilo koti na hizo kalamu.
0 Maoni/Comments:
Post a Comment